Mchezaji tenisi raia wa Uingereza, Andy Murray anatarajia kucheza na
Tennys Sandgren katika mzunguko wa kwanza wa michuano ya US Open.
Bingwa huyo mara tatu wa Grand Slam,Murray alishindwa kuirudisha nafasi
yake ya kwanza katika viwango vya ubora duniani mapema mwanzo mwa wiki
hii lakini pia akishindwa kuingia viwanjani tangu alivyofanya hivyo kwa
mara ya mwisho katika michuano ya Wimbledon alipo cheza na Sam Querrey
hatua ya nusu fainali na kupata majeraha.
Suluhu dhidi ya mmarekani, Sandgren ambaye yupo katika nafasi ya 104
duniani itatosha kumfanya Murray kuingia katika mzunguko wa pili wa
michuano hiyo na kukutana na mchezaji Rogerio Dutra Silva au Florian
Mayer. By Hamza Fumo
Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Salum
Mayanga ametangaza kikosi cha wachezaji 21 kwa ajili ya mchezo wa
kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Botswana utakao pigwa Septemba 2
mwaka huu.
Wachezaji hao wa Taifa Stars wanatarajia kuingia kambini Agosti 27
siku ya Jumapili saa mbili usiku nakuanza mazoezi tarehe 28 ya mwezi huu
tayari kwa maandalizi ya mchezo.
Kocha Mkuu wa timu hiyo, Salum Mayanga amesema “Tunategemea kuanza
kambi siku ya keshotarehe 27 saa mbili usiku hapa hapa Dar es salaam na
tunategemea kuwa na vijana 21 kambini ambao watafanya mazoezi sikua ya
Jumatatu jioni na kumaliza mazoezi tarehe 1 na siku inayofuata ndiyo
mchezo wetu na Botswana katika uwanja wa Uhuru”, amesema Mayanga.
Kwa upande wake Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania, Alfred Lucas amesema “Kutakuwa na mabadiliko ya ratiba
ya ligi kwa sababu tulitarajia zaidi kwamba tarehe za FIFA zisianze
tarehe 28 tulitegemea zingeanza baadaye lakini wao wametuletea taarifa
nafikiri ilikuwa wakati ule wa uchaguzi ambao kidogo wameturudisha nyuma
tuliamini ingekuwa tarehe tano na kuendelea la kini wao wamerudisha
tena nyuma”.
Msanii wa Bongo Flava, Matonya ameelezwa kushangazwa na WCB kutoa
wimbo ‘Zilipendwa’ jina ambalo ameshalitumia katika ngoma yake.
Kupitia
mtandao wa Instagram Matonya ametoa pongezi kwa kile kilichofanyika ila
hajapendezwa na kitendo cha kutokupewa taarifa hadi ngoma hiyo kutoka
kwani ana haki zake katika jina hilo.
Nduguzangu wasafi / Nawapongeza sana kwa kazi mzuri mnazo
zifanya / Nilifurahi Sana mlichokifanya kwa saida karoli dadaetu/
mlimuita mkamshirikisha akawapa Baraka zake/ kwangu mlishindwa nini?
Sina shida Ya Pesa nina shida Ya heshima cose najua dunia ni mapito/
kama mimi naibiwa haki yangu vipi wasanii wachanga? Basata mkowapi?
Wadau Wa muziki mkowapi? Usipo ziba ufa tajenga kuta!! Khaaa tena Bila
wogalakini haki itafata mkondo wake.
Hapo jana wasanii wote wa WCB yaani Diamond Platnumz, Rayvanny, Rich
Mavoko, Queen Darleen, Lava Lava, Harmonize na Maromboso aliungana kwa
pamoja na kutoa wimbo ‘Zilipendwa’ ambao kwa sasa umekuwa gumzo kila
kona.
By Peter Akaro
Mabingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation
Cup) na Ngao ya Jamii, Simba SC imechomoza na ushindi mnono wa mabao
7-0 mbele ya Ruvu Shooting mchezo uliyopigwa katika dimba la Uwanja wa
Uhuru.
Katika mchezo huo Simba ilitakata katika dakika 45 za kipindi cha
kwanza na kupelekea kuchomoza na mabao 5-0 katika kipindi hicho ambapo
mchezaji kipenzi cha mashabiki wa wekundu wa msimbazi Simba mganda
Emmanuel Arnold Okwi akionyesha maajabu ya kucheka na nyavu.
Magoli ya Simba yamefungwa na Emanuel Okwi katika dakika ya 21 , 22
na 35 wakati bao la nne likifungwa na Shiza Ramadhani Kichuya kunako
dakika ya 42 ya mchezo wakati la mwisho ambalo ni la tano katika kipindi
cha kwanza likifungwa na mchezaji Juma Liuzio kunako dadika ya 46 kabla
ya muamuzi kupiga kipyenga kuashiria mapumziko.
Katika kipindi cha pili cha mchezo huo wekundu wa msimbazi Simba SC
ikajipatia mabao mawili yaliyofungwa na mchezaji wao Okwi pamoja na
Erasto Nyoni hivyo kuufanya mchezo huo kumalizika kwa jumla ya mabao
7-0. By Hamza Fumo
Msanii wa Bongo Flava, Chin Bees chini ya Wanene Entertainment
ameachia video ya ngoma yake mpya ‘Kababaye’, Video ya ngoma hii
imeongozwa na Destro.
By Peter Akaro